24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

CCM KUFANYA KAZI KWA BIDII

Na ELIUD NGONDO, CHUNYA

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Michael Chonya amewataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii ili kwendana na kasi ya Rais Dk.John Magufuli.

Hayo ameyasema jana, wakati wa uchaguzi viongozi wa chama hicho Kata ya Matundasi wilayani humo.

Alisema viongozi wanatakiwa kutekeleza kwa kutumia hotuba za Rais Dk. Magufuli, alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema wanatakiwa kuzingatia utendaji kazi ambao unalenga kuwasaidia wananchi wa kawaida na si kufanya kazi kwa maslahi yao binafsi.

“Ahadi ya tano ya mwana TANU, inasema ‘cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu’ hivyo sisi tuliopewa dhamana ni lazima tuzingatie hili,” alisema Chonya.

Katika uchaguzi huo, Chonya alimtangaza, Edson Kibusu, kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa Kata ya Matundasi  kwa kupata kura 88 na  dhidi ya mpinzani wake, Eliji Salumu, ambaye alipata kura nane.

Viongozi wengine waliochaguliwa, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata, nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya na nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa.

Baada ya uchaguzi huo, Kibusu alisema ushindi alioupata sio wa kwake, bali ni wa wanachama wote wa chama hicho Kata ya Matundasi.

Alisema kwa kufuata misingi ya chama, yeye na viongozi wa ngazi za matawi na mashina ambao tayari wamepatikana, watafanya kazi kwa nguvu ili kuhakikisha wanakisimamia chama vema kwa manufaa ya wananchi wote.

“Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, kwa hiyo kazi yetu ni kuibua changamoto zinazowakabili wananchi kwenye kata yetu na kuziwasilisha kwenye Serikali kwa ajili ya utatuzi, zipo changamoto za maji, afya na miundombinu ya barabara,” alisema Kibusu.

 

Kwa upande wake, Diwani wa kata hiyo, Kimo Choga, alisema kila kiongozi wa chama hicho asijichukulie kuwa ni mheshimiwa,badala yake wajione watumwa wa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles