Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC), Deogratius Ruta, amewataka viongozi wa chama hicho mkoni Kilimanjaro kuhakikisha kwamba wanaendeleza Umoja na Mshikamano.
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 17,2021, wakati akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Seleman Mfinanga, ambaye alipata kura 43 kati ya 48 zilizopigwa.
Ruta amewataka viongozi hao pamoja na viongozi waliochaguliwa kushika nafasi hizo kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama ikiwa ninpamoja na kuwaona na kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kutatua changamoto zao.
Amesema chama kinajengwa na ajenda ya vikao na kuwataka suala la msingi ndani ya chama kipaumbele cha kwanza kijengwe kwa vikao, kwasababu chama kinajengwa na vikao na hivyo akawasihi viogozi hao waliochaguliwa kujenga mshikamano.
“Chama niwanachama na hawapatikani barabarani jengani mshikamano na umoja, hii ndio iwe agenda ya vikao vyenu,”amesema Ruta.
Akizungumzia hali ya chama Ruta amesema kwa sasa kipo kwenye hali nzuri kutokana na kushinda ushindi wa kishindo kwa uchaguzi wa Mkuu wa mwaka jana ambapo Mkoa walifanikiwa kuyakomboa majimbo yote yaliyokuwa upinzani.
Akitoa nasaha zake mara baada ya kutangazwa mshindi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Suleman Mfinanga, amewashukuru wajumbe hao na kuahidi utumishi uliotukuka na pia amesema atashirikiana na kila mmoja kwa ajili ya kazi za chama.
Awali akizungumza Mjumbe wa MNEC aliyemaliza muda wake, Joseph Tadayo ambaye amesema kuwa kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha wanakwenda kuwatumikia wananchi.
“Tunahitaji kwenda mbele kwa kuwataumikia wananchi kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika majimbo yetu na kusikiliza kero za wananchi, na ndiyo njia pekee ambayo imekiwezesha chama kuendea kushinda chaguzi zote ambazo zimekuwa zikifanyika ndani ya chama,”amesema Tadayo..
Katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya MNEC ulikuwa inagombewa na watu watatu, ambao ni Suleman Mfinanga aliyepata kura 43, Rashid Mjeja(4) na David Kijo(1).
Aidha katika mkutano huo pia ulifanyika uchagauzi wa Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Mkoa, ambapo Selemani Swalehe ameibuka mshindi kwa kupata kura(28) akifuatiwa na Paul Maile aliyepata kura 20.