23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Watendaji Suma JKT watakiwa kufanyakazi kwa ufanisi

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulinzi Suma JKT GARD LTD anayeshughulikia Operesheni za Kibiashara, Luteni Kanali, Erasmus Bwegoge, amewataka Watendaji wa Suma JKT kuhakikisha wanafanya kazi kwa Ufanisi, weledi na Uaminifu ili kusaidia kuleta tija katika shughuli za kujenga Taifa.

Akitoa agizo mapema leo jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari 6 ya Kampuni ya Ulinzi Suma JKT ambapo amesema Magari hayo yaliyonunuliwa yatasaidia kuondoa changamoto ya upungufu wa magari na kuongeza ufanisi katika utendaji shughuli za ulinzi

“Wasimamizi wa mali hizi wahakikishe magari haya yanatunzwa vizuri na yanatumika kwa lengo lililokusadiwa ili kuwa chachu kwa watendakazi na kuongezeka mapato kwa kampunim”mesema Kanali Bwegoge.

Aidha, amesema Suma JKT imekuwa ikijitahidi kununua vitendea kazi vya kutosha ikiwemo pikipiki na mashine hivyo mpaka kufikia mwaka huu wana magari 39 na gari moja liko njiani linakuja.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Suma JKT anayeshughulikia Operesheni za kibiashara, Luteni Kanali, Joseph Masanja, amesema kampuni hiyo ya ulinzi ilizinduliwa mwaka 2010 ikiwa na watendaji Saba lakini kwa sasa imeendelea na kufikia watendaji elfu kumi na tatu hivyo ni mafanikio mazuri.

“Magari sita yaliyozinduliwa yamenunuliwa kwa gharama ya thamani ya fedha Sh bilioni 2.9 na fedha zote zimeshakwisha kulipwa,”amesema Masanja.

Ameongeza kuwa watahakikisha vifaa wanavyovipata wanavitumia ipasavyo kuhakikisha shughuli zao zinaleta tija kwa Taifa katika kuhakikisha Ulinzi unaimarika kila mahali na usalama wa Wananchi na mali zao huku wakiishi kwa amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles