24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Dodoma yawatahadharisha wanaompinga Rais Samia

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimewasha moto kwa wale wote ambao wanapingana na Rais Samia Suluhu Hassan katika masuala ya maendeleo  huku kikidai makundi yanayowania urais mwaka 2025 ni ya wasaliti na wamejaa  tamaa ya madaraka.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukkasa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia jana Jumanne Januari 4, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan kudai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wamekuwa wakimsaliti katika suala la nchi kukopa.

Rais Samia alisema lazima nchi ikope kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwakuwa fedha za tozo haziwezi kutekeleza mahitaji ya miradi hiyo.

Amesema mkopo ambao Serikali umeupata wa Sh Trilioni 1.3 ni mzuri na haujawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru.

Akizungumza kwa niaba ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Januari 5,2022, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukasa amewawashia moto wale wote ambao wanapingana na Rais Samia katika masuala ya maendeleo

Dk. Mukassa alikuwa akimpongeza Rais kwa  hotuba yake aliyoitoa Januari 4 jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa ya Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma amemwomba Rais Samia kufanya kazi bila woga na kuachana na baadhi ya watu ambao wana uchu wa madaraka.

Dk. Mukassa ametoa wito kwa Wanaccm kuacha majungu, fitina na roho mbaya, kuacha kuharibiana kwani rais ni mmoja na hivyo aheshimiwe.

Katika hatua nyingine amelaani makundi yanayowania  Urais kwa mwaka 2025 kwani huo ni usaliti na tamaa na badala yake wamuunge mkono Rais katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles