25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Cannavaro, Yondani wapewa uchawi wa Kiongera, Tambwe

Maximo
Kocha mpya wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Marcio Maximo

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

KOCHA wa timu ya Yanga Mbrazil, Marcio Maximo, ni kama amesikia ubora wa washambuliaji wa Simba SC, Paul Kiongera na Amisi Tambwe, hivi sasa ameanza kuwapa programu maalumu mabeki wake wa kati, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani, kuhakikisha wanakabiliana na mashambulizi yoyote ya timu pinzani.

Mshambuliaji mpya wa Simba, Kiongera ambaye ni Mkenya, anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira, kufunga na kugawa mapande ya mabao ‘assist’, ambapo kwenye mechi yake ya kwanza tu dhidi ya Zesco United ya Zambia waliyofungwa mabao 3-0, alifanikiwa kushirikiana vema na Mrundi Tambwe.

Hivyo inaifanya safu hiyo ya ushambuliaji ya Simba kuwa kali, ikizingatiwa Tambwe alitisha sana msimu uliopita baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa mabao yake 19 aliyofunga.

Kwenye mazoezi hayo maalumu ya mabeki ya jana, yaliyokuwa yakisimamiwa na kocha msaidizi wa Yanga, Mbrazil Leonardo Neiva, mabeki wa kati walihenyeshwa vilivyo kwa kupigiwa mipira ya juu na ya chini, waliyotakiwa kuokoa vyema na kutoka kwenye eneo lao la 18.

Cannavaro na Yondani wao ndio walikuwa wakisimama pamoja na kuokoa mipira waliyokuwa wakipigiwa pembeni na ya juu, huku kundi jingine lilikuwa na mabeki wengine wa kati, Rajab Zahir na Pato Ngonyani, ambao nao walikuwa wakitakiwa waokoe kama wenzao, mabeki wa pembeni walikuwa ni Oscar Joshua na Juma Abdul.

Kwa mujibu wa programu hiyo, inamaanisha Maximo anawaandaa mabeki wake kukabiliana na aina yoyote ya mashambulizi yatakayofanywa na timu pinzani, ili kuzuia timu yake kufungwa mabao ya kizembe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles