LIMA, PERU
BUNGE la Peru hapo limepiga kura ya kuanza kwa shauri la kutokuwa na imani na Rais Martin Vizcarra, ambalo linaweza kumsababishia ang’olewe madarakani kutokana na kile kinachiotajwa “kutokuwa na maadili.”
Kwa mujibu wa gazeti la Comercio, katika mchakato wa kupiga kura ya kutoa ridhaa ya kuanza mchakato wa mashtaka wabunge 65 walipiga kura ya ndio na 36 hapana huku 24 wakiwa hawakushiriki. Vizcara anatuhumiwa kuwataka washauri wake kusema uongo katika uchunguzi uliokuwa ukiendeshwa na bunge.
Rais mwenyewe ameiita hatua hiyo kuwa ni njama dhidi ya demokrasia.
Uchunguzi huo ulikuwa ukihusu mkataba tata wa mwimbaji wenye thamani ya dola milioni 50,000.
Kwa upande wake Polisi ya Ujerumani imesema imefanikiwa kukamata silaha za moto 250 na risasi elfu kadhaa kwa mtu ambae inaaminika kuwa ni mfuwasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia. Jeshi hilo katika jimbo la Lower Saxony limesema silaha hizo zimepatikana baada ya msako wake wa juzi jioni katika eneo la Seevetal, umbali mfupi kutoka katika jiji la Hamburg.Â
Taarifa ya polisi inasema wachunguzi wanadhani ana itikadi ya mrengo wa kulia “Kwa mazingira jumla ya uchunguzi” ingawa pia taarifa hiyo haijafafanua au kueleza kwa nini mtuhumiwa ameweza kuwa na silaha, jambo linalochochea uchunguzi unaoendelea kuhusu hisia za ukiukaji wa sheria ya silaha.
Katika miaka ya hivi karibuni vurugu za wenye mrengo mkali wa kulia nchini Ujerumani zimesababisha ongezeko la wasiwasi mkubwa.