27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Iran yalaani Bahrain kuhalalisha uhusiano na Israel

TEHRAN, IRAN

IRAN imeilaani vikali Bahrain kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel. Ikulu ya Marekani juzi ilitangaza mpango wa Bahrain, ikiwa ni takribani wiki nne baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu kufikiwa makubaliano yenye kufanana na hayo na Israel. 

Pande hizo tatu zinatarajiwa kushiriki hafla ya wiki ijayo ya mjini Washington. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, wizara ya mambo ya nje ya Iran imeeleza;

 “Ni uamuzi wa aibu na mbaya ambao utaingia katika rekodi za vitendo vya kashfa.” 

Wizara hiyo imeituhumu Israel kwa kuyaweka rehani maumivu ya muda mrefu ya Wapalestina kwa kile ilichoeleza sababu za kampeni za kutafuta kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump wa Marekani. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na shirika la habari la Isna, watu wa Palestina na ulimwengu wa Kiislamu kamwe hawatakubali kitendo cha kuhalalisha uhusiano na Israel.

Wakati huo huo, Uturuki imetangaza kwamba itafanya mazoezi ya kijeshi ya majini katika eneo la pwani ya Cyprus licha ya tishio linalowakabili la vikwazo vya Umoja wa UIaya. 

Uturuki ipo katika mvutano na Ugiriki unaohusu raslimali ya gesi na mafuta pamoja na ushawishi katika eneo la bahari la kusini ya Mediterania, jambo ambalo limezusha hofu ya kutokea mzozo mkali zaidi. 

Katika taarifa iliyotolewa na chombo kiitwacho NAVTEX, Uturuki imesema kutakuwa na mazoezi ya matumizi ya bunduki za risasi za moto katika eneo la pwani la Sadrazomkoy, kaskazini mwa Cyprus. 

Tangazo hilo limetolewa baada ya hapo Alhamis viongozi wa mataifa ya kusini mwa Ulaya kuonya kwamba, wako tayari kuunga mkono vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Uturuki kama serikali yake itakwepa mazungumzo. 

Suala hilo pia litajadiliwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wa Septemba 24 hadi 25.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles