27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

BOT YATOA GAWIO LA BILIONI 300/- KWA SERIKALI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM –


BODI ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeidhinisha gawio la Sh bilioni 300 kwa Serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, ilieleza kuwa kiasi hicho cha fedha kinafanya gawio la BoT katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2014/15 hadi 2016/17 kuwa Sh bilioni 780 ambapo kwa mwaka 2014/15 ilitoa gawio la Sh bilioni 180 na mwaka 2015/16 gawio la Sh bilioni 300.

“Kifungu cha 18 (5) cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaipa Benki Kuu mamlaka ya kutoa gawio kwa Serikali pale inapotengeneza faida.

“Majukumu ya msingi ya Benki Kuu sio kutengeneza faida; hata hivyo, inapotokea kwamba faida imepatikana, sehemu kubwa hutolewa kama gawio kwa Serikali.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa,” ilieleza taarifa hiyo

Mbali na hayo alisema majukumu mengine ya BoT ni kuchapisha noti na sarafu za Shilingi ya Tanzania,  usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha, kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo ya taifa,  kuhifadhi akiba ya fedha za kigeni ya taifa,  kutoa ushauri wa kiuchumi na fedha kwa Serikali ya Muungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. “Majukumu ya msingi ya Benki Kuu sio kutenfeneza faida” – Hiyo faida ambayo imetengenezwa imetokana na majukumu ganiambayo hayapo katika malengo ya uanzishwaji wake?
    Hapo Gavana unatuchanganya; au unarudisha fedha za bajeti mlizopewa na Serikali kama Bunge lilivyofanya?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles