28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BOT YAPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

 Na MWANDISHI WETU –Dar es Salaam                |                


BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imepunguza kiwango cha riba ya mikopo kwa benki zote nchini kutoka asilimia tisa hadi saba.

Taarifa ya BoT kupunguza riba hiyo iko katika barua yake ya Agosti 23, mwaka huu kwenda kwa benki zote ikizitaarifu juu ya uamuzi huo.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba GA 302/389/01 iliyosainiwa na Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha, Yamungu Kayandabila, imezitaarifu benki kuhusu punguzo la riba na utekelezaji wa uamuzi huo utaanza kutumika rasmi kuanzia kesho.

Imefafanua kusudio la kufikia uamuzi huo ni kuongeza kiwango cha ukopaji ili kusaidia shughuli za kiuchumi.

Akitoa maoni kupitia akaunti yake ya Twitter jana, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema: “Naona Benki Kuu imeshusha tena ‘discount rate’ ili kuziwezesha benki kuwa na fedha zaidi za kukopesha watu na kampuni.

“Hii ni mara ya tatu BoT inachukua hatua hiyo, lakini matokeo ni sifuri. Tunawakumbusha uchambuzi wetu wa Oktoba, 2017 kuwa uchumi unasinyaa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles