25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bonnah asema miaka mitatu ya Samia kielelezo cha mafanikio nchini

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli amesema maendeleo yaliyofanyika katika jimbo hilo na maeneo mengine chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ni kielelezo cha mafanikio makubwa yaliyofikiwa nchini.

Bonnah ameyasema hayo Machi 23,2024 wakati wa kongamano aliloliandaa kutathmini miaka mitatu ya Rais Samia ambalo limeshirikisha wanawake kutoka katika kata 13 za Jimbo la Segerea.

Ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika jimbo hilo kuwa ni uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii kama vile afya, elimu, miundombinu ya barabara na madaraja na kuwawezesha wananchi kupata maendeleo.

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, akizungumza wakati wa kongamano aliloliandaa kutathmini miaka mitatu ya Rais Samia lililoshirikisha wanawake kutoka katika kata 13 za jimbo hilo.

“Mama yetu katika uongozi ana miaka mitatu lakini jimbo letu tumeongeza sekondari, watoto wetu wengi walikuwa wanasoma maeneo ya mbali na wanakoishi. Tunamshukuru amehakikisha kwamba kila kata inakuwa na shule ya msingi na sekondari na baadhi ya maeneo watoto wetu wanasoma ndani ya kata zao,” amesema Bonnah.

Amesema pia katika kata mbalimbali kama Liwiti, Bonyokwa na Minazi Mirefu wanaendelea na ujenzi wa shule za sekondari kwa mtindo kwa ghorofa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akizungumza wakati wa kongamano la kutathmini miaka mitatu ya Rais Samia lililoandaliwa na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli.

Mbunge huyo amesema ujenzi wa vituo vya afya umetekelezwa katika kata ambazo hazikuwa na vituo ikiwemo Kinyerezi, Kiwalani, Mnyamani na kwamba watahakikisha zingine zenye zahanati zinaongezewa uwezo ziwe na vituo na ambazo hazina kabisa zipate zahanati.

“Miundombinu ya barabara bado si mizuri lakini tunawaomba wananchi waendelee kuwa wavumilivu awamu ya pili ya Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (DMDP) utaaanza kutekelezwa hivi karibuni na tunatarajia utamaliza kero hiyo,” amesema.

Hata hivyo amesema licha ya elimu kutolewa bure bado watoto wamekuwa wakitakiwa kwenda na fedha shuleni jambo linalolalamikiwa na wazazi wengi.

“Maisha ni magumu unakuta mama ana watoto sita je, akiambiwa wote waende na fedha ataweza…tunaomba sana suala hili liishe kwa sababu Serikali ilishatangaza elimu inatolewa bure,” amesema Bonnah.

Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumike Malilo, amesema kata hiyo ilikuwa haina barabara za lami lakini hivi sasa zimeanza kujengwa ikiwemo ya kutoka Kinyerezi – Bonyokwa – Kimara huku kero ya maji ikielekea kupata ufumbuzi.

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, amesema jimbo hilo lina maendeleo makubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma na kumpongeza Bonnah kwa kazi nzuri anayofanya.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Neema Kihusa, amesema; “Mama Samia anahangaika kulitangaza taifa letu, tunapata miradi mikubwa nawaomba wanawake tunapoingia kwenye uchaguzi tupiganie 50 kwa 50, tusiogope, tupendane tukavunje ile dhana kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke.

“Tukiwa kitu kimoja hata wanaume watakuwa mstari wa mbele kutuunga mkono, wanaume mtuunge mkono wanawake tunaweza,” amesema Kihusa.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amempongeza Bonnah kwa kuwaunganisha wanawake kutoka katika makundi mbalimbali na kuahidi kuendelea kushirikiana naye kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo.

Amesisitiza kuwa elimu inatolewa bure na kuwatahadharisha walimu wanaochangisha wazazi fedha kwamba watachukuliwa hatua huku akiwataka wazazi kutoa taarifa iwapo watatakiwa kutoa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles