23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bongo Fleva wakacha Tamasha la Sanaa Bagamoyo

BONGO FLEVANA FESTO POLEA

TAMASHA la 34 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililoanzishwa mwaka 1981 na Chuo cha Sanaa Bagamoyo (kwa sasa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo), linatarajiwa kufanyika kwa siku sita katika viwanja vya chuo hicho bila ya kuwa na ushiriki wa wasanii wa Bongo Fleva.

Mwenyekiti wa Tamasha hilo, John Mponda, alilieleza MTANZANIA kwamba hakuna msanii wa Bongo Fleva yeyote aliyejitokeza kuomba kushiriki katika tamasha hilo, jambo ambalo linaonyesha kutokuwa na wasanii hao katika tamasha hilo.

“Tamasha hilo litaanza Septemba 21 hadi 27, likiwa na kauli mbiu kwamba ‘Sanaa na Utamaduni katika Uchaguzi huru na wa Amani’ na pia tunawakaribisha wasanii wa bongo fleva wajitokeze kwa kuwa muda bado upo,’’ alieleza Mponda.

Mwenyekiti huyo alisema licha ya wasanii hao kutojitokeza, lakini idadi kubwa ya vikundi vya ngoma za asili, maigizo, sarakasi, mazingaombwe, muziki wa kisasa na asili, sanaa za ufundi na bidhaa mbalimbali vitatoa burudani kupitia kazi zao.

Aliongeza kwamba vikundi 48 vimethibitisha kushiriki, ambapo ni vikundi 43 vya Tanzania na vikundi vitano kutoka nchi ya Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.

Licha ya tamasha hilo kuwa la burudani, pia kutakuwa na mada ndogondogo zitakazotolewa kupitia kongamano na warsha zitakazohusu haki za binadamu, rushwa na kupinga mauaji ya albino.

Tamasha hilo lilianzishwa ili kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo hicho kuonyesha kwa vitendo waliyojifunza kwa mwaka mzima kwa kushirikisha wakazi wa maeneo hayo, lakini baadaye likabadilishwa na kuwa tamasha la kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles