Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, amewataka wananchi wote waliojenga juu ya miundombinu ya maji wabomoe nyumba zao kwa kuwa ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Mbarawa aliwataka watendaji wake kuhakikisha wanasimamia sheria na kuwaondoa watu hao.
“Kwa mwananchi aliyejenga ndani ya maeneo ya miundombinu ya maji sisi tutabomoa tu kwa kuwa sheria iko wazi, sisi kama Serikali tutalisimia hili,” alisema Profesa Mbarawa.
Alisema ikitokea bomba linalopitisha maji kwa mgandamizo mkubwa likipasuka, wananchi walio kwenye eneo hilo watapoteza maisha, hivyo kabla ya hilo halitokea wataondolewa.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.