Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
DREVA Pikipiki maarufu ‘Bodaboda’ mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, Rashid Ally Handiko, amefanikiwa kushinda Sh milioni 10 za bahati nasibu ya Watanzania Biko kwa kupitia droo yake kubwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikiwa ni mwendelezo wa watu wengi kuendelea kushinda mamilioni ya zawadi kutoka kwenye bahati nasibu hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 12, 2022 katika makabidhiano hayo, Ally amesema amefarijika kuona ameshinda fedha sanjari na kukabidhiwa kwa haraka kiasi cha kuamua kitu cha kuzifanyia kwa ajili ya kuendeleza maisha yake.
“Nashukuru kufanikiwa kushinda fedha zangu na kukabidhiwa bank kwa haraka kwa maana ndio njia ya kuzipatia kazi ya kufanya, ukizingatia kuwa hii njia nzuri ya kukuza uchumi wangu,” amesema Ally.
Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia Sh 2,500 hadi Sh milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.
Kianzio cha kucheza Biko ni Sh 1,000 na kuendelea ambapo Watanzania wengi wameendelea kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za kushinda hadi Sh milioni 40, zikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wote wanaocheza Biko.
Droo za biko zinafanyika kila Jumapili ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakishinda zawadi kubwa za wiki bila kusahau papo kwa hapo zinazoingia moja kwa moja kwenye simu za mkononi.