24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bob Junior aanzisha utoaji wa albamu

Bob JuniorNA ESTHER GEORGE

BAADA ya kimya kirefu katika muziki, msanii na prodyuza wa muziki wa Bongo Fleva, Raheem Rummy maarufu kwa jina la Bob Junior, ameanzisha mfumo wa utoaji albamu kwa wasanii waliopo katika studio yake ya Sharobaro records.

Sharobaro ameanza mfumo huo kwa kutoa albamu yake mpya ya ‘Ukweli Wangu’ yenye jumla ya nyimbo 18 ikiwa muda mrefu umepita tangu wasanii wakache albamu kwa madai ya kutokuwa na soko.

Bob Junior alisema kwa muda mrefu amekuwa kimya na sasa ameamua kuibuka na albamu kamili yenye nyimbo nyingi badala ya kutoka na wimbo mmoja mmoja kama wafanyavyo wasanii wengi wa muziki huo.

“Kimya changu cha muda mrefu ilikuwa ni kuandaa vitu vizuri kwa mashabiki wangu na sasa nimerudi kwa kazi nyingi mpya kutoka kwangu na wasanii waliopo chini ya studio yangu ya Sharobaro records,” alisema Bob Junior.

Katika albamu hiyo amewashirikisha mastaa kutoka nje ya nchi akiwemo Tecno wa Nigeria, Chameleon wa Uganda, Roma na wengine wengi wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles