23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Binti ya miaka 15 atumia bunduki ya AK-47 kuokoa familia yake

KABUL, AFGHANISTAN 

NYUMBA yao ilipovamiwa mwezi uliopita, Nooria mwenye umri wa miaka 15, alichukua bunduki ya AK-47, na kuua wanaume wawili na kumjeruhi wa tatu.

Alisifiwa kwa kuwa shujaa. Lakini kinachokanganya zaidi ni kile kilichotokea usiku huo.

Majina yote yamebadilishwa kwa sababu za kiusalama.

Inaelezwa wanaume hao waliingia kijijini humo usiku wa manane kukiwa na giza totoro.

Kulingana na Nooria, ilikuwa ni karibu saa saba usiku walipoingia kupitia mlango wa mbele nyumbani kwa wazazi wake.

Akiwa kwenye chumba chake, kijana huyo aliyeamshwa na kelele zilizokuwa zinaendelea, alikaa kimya na mkakamavu. Alifikiria kaka yake wa miaka 12 ambaye yuko kwenye chumba chake.

Kisha akasikia wanaume hao wakiwachukua wazazi wake na kuwatoa nje kuliko na nyumba ndogo eneo la milimani. Anaelezea tukio hilo katika mahojiano na BBC.

Kitu kilichofuata, akasikia milio ya risasi, anasema.

“Waliwaua.”

Noori amekulia eneo la kijijini huko Afghanistan.

Alikuwa msichana mwenye haya na mkimya, lakini alijua kutumia bunduki na kufyatua risasi sahihi – jambo lililokuwa kama ulinzi wake baada ya kupewa mafunzo hayo na baba yake akiwa na umri mdogo.

Usiku huo, badala ya kujificha, Nooria alichukua bunduki ya baba yake – aina ya AK-47 – kisha akafyatulia risasi wanaume hao waliokuwa nje ya nyumba yao. Alipiga risasi hadi akakaribia kuzimaliza zote, anasema.

Hatimae, karibia saa moja tangu walipowasili, wanaume hao walisalimu amri, anasema.

Nje ya nyumba yao kulikuwa na miili ya wanaume watano: ule wa mama yake na baba yake, mwili wa jirani yao mzee ambaye alikuwa jamaa yao na miili ya washambuliaji wawili.

“Hali ilikuwa inatisha,” amesema. “Walikuwa wakatili. Baba yangu alikuwa mlemavu. Mama yangu hakuwa amefanya lolote. Na wakawaua tu bila sababu.”

Nooria alihamishwa kutoka nyumbani kwao hadi eneo salama Kabul.

Kukulia Afghanistan, watoto vijana kama Nooria hawajui kingine chochote zaidi ya vita.

Mgogoro unaoendelea kati ya vikosi vinavyopendelea serikali na Taliban, wanamgambo wenye msimamo mkali umekuwepo kwa zaidi ya miaka 25.

Vikosi vinavyopendelea serikali vinadhibiti miji mikubwa huku kundi la Taliban likitwaa maeneo ya vijijini. Vijiji kama vya Nooria mara nyingi hujikuta vimetumbukia kwenye mgogoro huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles