25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Binti wa Rais Regan alaani baba yake kuwaita Watanzania tumbili

WASHINGTON, MAREKANI

MTOTO wa kike wa rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan amesemavhakuna la kujitetea  kutokana na kauli aliyoitoa baba yake mwaka 1971 katika mazungumzo ya simu akiuelezea ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kama “tumbili”.

Mkanda mpya wa sauti ndio uliofichua kuwa  Reagan akisema hayo wakati huo akiwa Gavana wa California.

Binti yake,  Patti Davis amelaani vikali katika waraka wake uliochapishwa katika gazeti.

“Hakuna la kujitetea ,hakuna ufafanuzi wa maelezo, hakuna ufafanuzi mzuri juu ya kile ambacho baba yangu alikisema ,” aliandika.

Davis aliandika katika waraka kwa ajili ya gazeti la Washington Post kwamba alikuwa anajiandaa kumtetea baba yake kabla ya kusikia kanda ya sauti, lakini alishituka baada ya kusikia kile alichokisema rais huyo wa zamani.

“Siwezi kuwaambia kuhusu mwanaume aliyekuwa akiongea kwa simu…si mwanaume niliyemfahamu mimi,” aliandika

Sauti iliyorekodiwa hivi karibuni ilionekana kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Atlantic.

Reagan alitoa kauli katika mazungumzo na rais wa Marekani aliyekuwa madarakani wakati huo  Rais Richard Nixon.

Ronald Reagan aliuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kama ”tumbili”

Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa(UN), ambao walikuwa upande wa wapinzani wa Marekani katika kura dhidi ya kuitambua Uchina na kuiondoa Taiwan katika Umoja wa Mataifa.

Reagan – ambaye alikuwa anaiunga mkono Taiwan – alimpigia simu rais siku iliyofuata akimwambia : “Aaangalie hao … tumbili kutoka hizo nchi Afrika – ambao bado hawafurahii kuvaa viatu,”.

Nixon anasikika kwenye mkanda huo akiangua kicheko kwa sauti kubwa baada ya kauli hiyo.

Ronald Reagan alikuwa rais wa Marekani kuanzia mwaka 1981 hadi 1989

Yeye mwenyewe pamoja na kuwaita Watanzania tumbili aliwahi kuandika jinsi alivyopambana dhidi ya ubaguzi alipocheza soka ya chuoni na baadae alipoingia madarakani alipopewa uanachama wa klabu ya taifa ya ritzy mjini Los Angeles ambayo aliikataa kwasababu haikuwaruhusu Wayahudi au Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Binti yake aliandika kuwa maneno aliyoyasikia “Yatabaki nami daima, ” na  akaongeza kuwa kama baba yake angekuwa bado hai “angeomba msamaha ” kama angesikia sauti yake iliyorekodiwa kwa sababu  haiwezi kueleweka kwa maneno mengine isipokuwa ubaya.

Aliongeza kuwa anatumaini watu watamsamehe rais huyo wa zamani wa marekani “kwa maneno ambayo hayangepaswa kutamkwa katika mazungumzo yoyote yale.

Wakosoaji wanamshutumu Reagan kuwa mbaguzi wa rangi katika kipindi chake chote cha maisha ya kazi.

Alipokuwa akigombea kiti cha ugavana wa California mwaka 1966, mchezaji huyo wa zamani wa filamu alisema “kama mtu binafsi anataka kuwabagua waniga (Negroes) au wengine katika kuuza au kukodisha nyumba, ni haki yake kufanya hivyo “.

Hata hivyo Reagan alikanusha shutuma za ubaguzi wa rangi dhidi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles