24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 49.6 zatumika kutekelez miradi Sengerema

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wilaya ya Sengerema  iliyopo jijini hapa imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa bajeti ya Sh Bilioni 49.6  kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 kwenye halmashari hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Mipango wa Wilaya hiyo, Ndaro Samson, kwenye kikao cha mapendokezo na Mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/2022 kilichofanyika jijini hapa.

Samson alisema mpaka kufikia februari 28 mwaka huu halmashari ilikuwa imepokea Sh Bilioni 25.4 Sawa na asilimia 54.3  na matumizi ni  Sh bilioni 24.1 sawa na asilimia 52.1.

Alisema moja ya vipaumbele walivyojiwekea kwenye halmashauri hiyo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 14 kwa Shule za msingi na vyumba 18 vya Sekondari.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka watendaji wa halmashauri kuacha kufuata miongozo ya wizara badala yake waangalie uhitaji wa wananchi ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Wito huo  ulitolewa jana wakati akifungua kikao  hicho alisema kuwa muongozo wa wizara pekee hautoshi kukidhi uhitaji katika maeneo husika.

Alisema baadhi ya wanaoandaa miongozo hiyo hajawahi kukaa hata ngazi ya kijiji,  kata, au halmashauri, wanawezaje  kuelekeza ujenzi wa vyumba vya madarasa matano  huku uhitaji ukiwa ni madarasa zaidi ya hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles