25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONEA WA NYUMBA ZA LUGUMI AMALIZA KAZI

Ni kama sinema vile wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika Shirika la Posta ilipokatizwa ghafla na  Bilionea wa nyumba za Lugumi, Dk. Louis Shika aliyekuwa makini kwenye kompyuta upande wa huduma za kimtandao akidai kutuma fedha nchini Urusi ili aingiziwe fedha zake zilizopo nchini humo aweze kununua nyumba za Lugumi.

Awali, Dk. Shika alipoombwa kuzungumzia alichokuwa akifanya alikataa awali kwa madai kwa yuko ‘busy’ kufanya mihamala Urusi na tayari ametuma Dola 100.

Dk. Shika amesema awali alikuwa mjinga kwani hakuelewa nini anatakiwa kufanya ndiyo sababu akaamua kusema ataingiza fedha baadaye kumbe ni kosa.

Alipoulizwa kama hadi fedha za zake zifike nyumba za Lugumi zitakuwa zimenunuliwa, alijibu:  “Dar es Salaam nyumba zinazouzwa ni nyingi sana siyo mpaka za Lugumi, Mimi lengo langu ni kununua nyumba na si vinginevyo.”

Pamoja na mambo mengine, Dk. Shika amesema hatawashitaki waliomkamata na kumuweka ndani anamuachia Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles