LEO imenilazimu kuzungumzia suala la ‘cholesterol’. Hii ni kwa sababu jamii imekuwa haina ulewa wa kutosha kuhusu suala hili kwenye damu. Sitaingia kwa undani zaidi ili kila mtu anielewe na aweze kupata ufahamu.
Tangu nilipokuwa mtoto mdogo sikujua nani aliyesema mafuta yanasababisha magonjwa ya moyo, sikujua nani na mwanasayansi yupi aliyeteka ulimwengu hadi tukafikia hapa tulipo. Nilipofika chuo kikuu kila nikisoma sentesi, labda nasoma jinsi ya kumshauri mgonjwa wa kisukari nilikutana na sentensi kuu zifuatazo; acha mafuta, punguza uzito, fanya mazoezi. Endapo ukizidisha maswali nilikuwa naona daktari anakwambia mtembelee mtaalamu wa lishe.
Ukifika kwa mtaalamu wa lishe atakusikiliza kisha anakuandalia ‘Gazeti la mateso’ unajua kwanini naliita gazeti la mateso?
Kwa sababu anakuandalia mlolongo wa vyakula ambavyo wewe siku hiyo huna hamu navyo, eti kwa sababu una kiu ya kupungua ule tu hicho chakula.
Babu zetu hawakupangiwa vyakula kwenye makaratasi na walikuwa wenye afya bila vitambi, unapopangiwa chakula kunakuwa hakuna uhusiano mzuri na wenye furaha na chakula kilichopo mbele yako maana yake unakula kutokana na shida tu.
Anakupimia chakula ule gram ngapi na kalori kiasi gani. Kila mtu hapa mtaalamu wako hata angalia mwili wako unaumia kiasi gani yeye anachoangalia unapungua uzito au la! Yaani bora punda afe mzigo ufike. Bora uugue vidonda vya tumbo kwa malengo ya kutoa kitambi… ndio ni nzuri lakini ina gharama yake.
Babu zetu hawakuwa na mzani, sasa sijui walipima chakula kwa kutumia nini mpaka walikuwa na afya bora kiasi hicho?
Swali la kujiuliza, mbona ubunifu katika sayansi na teknolojia unaongezeka na maradhi ya lishe yanashamiri?
Hivi ni kwei Watanzania na dunia nzima hatujajua kula ili tuweze kuishi tukiwa na afya njema?
TAFAKURI
Hivi umeshawahi kuona mtu ana kilo 140 na bado anakula baga, pizza au soda? Ndio, mimi nimeshawaona unajua ni kwa nini wanafanya hayo?
Jibu ni kwamba; wamekata tamaa na elimu isiyozaa matunda. Wamejitesa na wamesumbuka hatimaye wameibua vidonda vya tumbo bila mafanikio.
Najua hata wewe umekata tamaa, basi hata mimi nilikata tamaa baada ya kujifunza haya nilijua nilikosea wapi.
Binadamu katika dhambi kubwa kuliko zote ni kuendelea kuongeza utamu wa sentensi; “Cholesterol ni adui yetu”
Kuanzia leo napenda kukuambia kwamba bila ‘cholesterol’ huna uhai hapo ulipo, bila ‘cholesterol’ usingekuwa unasoma sentensi hii ninayoandika.
Wengi watakwambia mwili wako unatengeneza cholestro hivyo huna haja ya kuupa tena. Kwani nani hajui sukari glucose hutengenezwa na ini hata kama usipokula wanga? Lakini mbona tunashauriwa kula hadi asilimia 60?
Hebu twende sambamba leo sote!
Kwa mafunzo mengi zaidi nitembelee kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa jina Dk. Boaz Mkumbo MD. Pia Tembelea tovuti yangu ya afya www.drboazmkumbomd.com
Itaendelea wiki ijayo.