30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Parachichi ndio malkia wa matunda

AvocadoNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUNDA la parachichi linafaida nyingi mwilini kiasi kwamba baadhi ya watu wamelipa jina la malkia wa matunda.

Kuna ambao wamethubutu kuliita parachini kuwa ni aina nyingine ya ndizi. Huko nyuma tunda hili halikuwa likizingatiwa sana lakini kutokana na faida zake kiafya na hata katika masuala ya vipodozi, hivi sasa ni miongoni mwa matunda yanayosifika zaidi duniani.

Tunda hili lina kiasi kidogo cha maji tofauti na matunda mengi tuliyozea kula, lina kiwango kikubwa cha mafuta na ndani yake pia kuna tindikali (acid) aina mbalimbali zinazosaidia kukinga na kutibu maradhi mwilini.

Parachichi pia lina kiwango cha juu cha protini na vitamini E. Inaelezwa kuwa, vitamini E iliyoko kwenye parachichi ni nyingi zaidi kuliko ile inayopatikana kwenye vyanzo vya wanyama. Kwamba hata mayai hayana kiwango kikubwa cha protini ikilinganishwa na parachichi.

Sifa hiyo inalifanya kuwa tunda linalopendwa kuliwa na wanamichezo hasa wale wanaopenda kujenga miili yao kwa kutumia ‘amino acids.’ Virutubisho vingine ni vitamini B6, madini ya chuma na madini ya potassium.

Parachichi ni chakula kizuri kwa watoto hasa kutokana na ulaini wake, virutubisho vilivyopo kwenye tunda hilo vinaweza kuwapa nafuu wale wenye matatizo ya mfadhaiko na matatizo ya uzazi kama ugumba na utasa.

Tindikali aina ya oleic iliyomo ndani ya parachichi inasaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na saratani. Pia linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwa kuwa lina ufumwele ambao ni muhimu katika kukinga kuta za utumbo. Wale wenye kusumbuliwa na ukosefu wa damu, kisukari, matatizo ya mfumo wa neva na mishipa ya damu wanashauriwa kula avocado mara kwa mara. Pia tunda hili limethibitishwa kupunguza kiwango kikubwa cha mafuta mabaya ya cholesterol kwenye damu hasa kwa watu  ambao ni wanene.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles