23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

BIFU ZILIZOTIKISHA MWAKA 2016

lil-wayne-cash-money-records-beef-x-birdman_lifeistremendez

NA BADI MCHOMOLO

TUKIWA kwenye mwezi wa mwisho wa mwaka 2016, katika safu hii ya zaidi ujuavyo, tutamaliza mwezi huu kwa kukukumbusha baadhi ya matukia ambayo yalifanywa na mastaa wan je ya nchi na kugusa hisia za mashabiki na wadau wa tasnia husika.

Tangu Januari 2016 hadi leo hii tupo Desemba, tunatarajia kukuonesha baadhi ya mabifu ambayo yalijitokeza kwa wasanii mbalimbali duniani na kugusa hisia za watu wengi.

Prezzo vs Jaguar

Tukianzia nchini Kenya, hapa tunakutana na wasanii wenye majina makubwa nchini humo ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki, Jackson Makini (Prezzo) na Charles Kanyi (Jaguar), hawa ni wasanii ambao wamekuwa hana maelewano kwa miaka mingi sasa kutokana na utofauti wa mafanikio waliyonayo.

Kila mmoja amekuwa akivutia kwake kwamba ana fedha nyingi kuliko mwenzake, kuna wakati bifu lao linapotea na kurudi, lakini Februari mwaka huu bifu hilo lilianza tena baada ya Prezzo kupewa nafasi katika runinga ya taifa ya KTN.

Msanii huyo alipata nafasi ya kuhojiwa na mrembo katika runinga hiyo ambaye anajulikana kwa jina Betty Kyallo, lakini Prezzo alishangaza watu baada ya kumtongoza mtangazaji huyo wakati kipindi kipo hewani.

Kutokana na kitendo hicho ambacho kilipingwa vikali na wadau mbalimbali kilimpa nafasi Jaguar kumshambulia msanii huyo na kudai kuwa atakuwa na matatizo ya akili, hivyo yupo tayari kutoa fedha zake kwa ajili ya kumpeleka ‘Rehab’ kwa ajili ya matibabu.

Hapo ndipo bifu la wawili hao likaanza kuwaka moto upya, hata hivyo Prezzo aliwahi kuulizwa kama anamjua Jaguar, lakini alijibu kuwa Jaguar anayomjua yeye ni mnyama ambaye anafanana na Chui pamoja na gari aina ya Jaguar lakini hakuna mtu ambaye anamjua anaitwa Jaguar.

Drake Vs Meek Mill

Inasemekana kwamba Aubrey Graham (Drake) na Robert Williams (Meek Mill), waliwahi kuwa marafiki wakubwa sana kipindi cha nyuma, lakini mwishoni mwa mwaka jana walianza kutofautiana kimya kimya kwa madai kwamba baada Drake kusikia Meek Mill anatoka na Nick Minaj.

Mapema mwaka huu Meek Mill alifunguka na kusema kwamba hana urafiki wowote na Drake kwa kuwa hajui kuandika mistari, huku akidai nyimbo nyingi anaandikiwa.

Kauli hiyo ilimfanya Drake aje juu na kudai kwamba Meek Mill anajifanya mjanja kwa ajili ya mpenzi wake Minaj ambaye hata yeye anatoka na mrembo huyo wakati huo Meek Mill akiwa kwenye ziara za muziki wake.

Bifu hilo linamaliza mwaka bila ya dalili zozote za kufikia mwisho, kila kukicha wawili hao wamekuwa wakishambuliana kwa maneno na inadaiwa kwamba Minaj ndio chanzo cha bifu hilo, huku Minaj akidai kuwa ataendelea kumpenda Meek Mill na watakuja kuoana.

Birdman vs Lil Wayne

Lil Wayne wakati anaingia kwenye tasnia ya muziki aliweka wazi kuwa Bryan Williams (Birdman) ni baba yake katika muziki kwa kuwa alimpokea na kumtambulisha katika tasnia hiyo huku akiwa na umri mdogo, lakini kwa sasa wawili hao hawapatani hata kidogo.

Chanzo cha bifu lao wawili hao inadaiwa kwamba Lil Wayne alikuwa na makubaliano na Birdman ambaye ni bosi wa Cash Money kwamba atampa Lil Wayne dola milioni 51 kwa ajili ya biashara yao ya muziki ambao wanaifanya katika kuendesha kundi hilo, lakini baada ya biashara kukamilika hakuna fedha yoyote ambayo alipewa rapa huyo.

Kutokana na kitendo hicho Lil Wayne aliamua kuondoka kwenye kundi hilo huku akiwa tayari amechafuana na bosi wake. Kwenye mitandao ya kijamii walirushiana maneno makali, lakini baada ya muda Birdman aliomba kuyamaliza huku akikubali kumlipa baadae, ila mambo yalikuwa tofauti hakuweza kufanya hivyo ndipo Lil Wayne akaondoka tena Agosti mwaka huu na kuanza kutishiana maisha, mwanzoni mwa wiki hii Lil Wayne alipanda kwenye staji jijini New York na kabla ya kumaliza kuimba alilitukana kundi la Cash Money na kushuka jukwaani.

Jay z vs Kanye West

Wamekuwa marafiki wa karibu sana kutokana na kufanya kazi pamoja, lakini leo hii urafiki wao umevunjika na hakuna maelewano tena. Inadaiwa walianza kugombana muda mrefu, lakini Oktoba mwaka huu mambo yao mengi yalikuwa wazi mara baada ya mke wa Kanye West, Kim Kardashian kuibiwa vitu nchini Ufaransa.

Inadaiwa tangu mrembo huyo aibiwe vitu vyake, Jay Z hakufanya lolote ambapo Kanye alitegemea kuona rapa huyo akiongea lolote hasa katika kutoa pole, mgogoro wao kwa sasa umezidi kuwa mkubwa ambapo hadi mke wa Jay Z, Beyonce amemtaka mume wake kuyamaliza na rafiki yake kwa kuwa ni jambo la aibu kwa wawili hao ambao walitamba na wimbo wa Otis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles