32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bibi Cup 2022 yawaunganisha Vijana Bukoba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Kijamii ya BIBI Trust ya Mjini Bukoba imedhamini Ligi ndogo ya mpira wa miguu ya Kombe la BIBI Cup 2022 katika Kijiji cha Rwanda Kata ya Ibuga Kamachumu mkoani Kagera.

Mkurugenzi wa Taasisi ya BIBI Trust, Teddy Rweyendera, akizungumza kabla ya kukabidhi Kombe kwa mshindi wa ligi ya BIBI Cup 2022 timu ya Bunene-Butundu baada ya mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga, Kamachumu mkoani Kagera juzi.

Ligi hiyo ilianza Agosti 20, mwaka huu kwa kushirikisha Vitongoji vinne katika Vijiji vya Busingo A, Busingo B, Kitunga-Kyamawa na Bunene-Butundu na kuhitimishwa Septemba 4 2022 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga iliyopo Kamachumu.

Ligi hiyo ya Bibi Cup 2022 imeitimishwa kwa mechi kati ya timu ya Kitunga-Kyamawa na Busingo B na matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao 2-2.

Mshindi wa ligi hiyo ni Bunene-Butundu ambayo imebeba Kombe, jezi, mpira mmoja na  fedha tasilimu Sh 50,000, mshindi wa pili ni Kitunga-Kyamawa, jezi,mpira na fedha Sh 25,000.

Mkurugenzi wa Taasisi ya BIBI Trust, Teddy Rweyendera, akizungumza kabla ya kukabidhi Kombe kwa mshindi wa ligi ya BIBI Cup 2022 timu ya Bunene-Butundu baada ya mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga, Kamachumu mkoani Kagera juzi.

Ligi hiyo imeanzishwa na wajukuu wa Bibi Yustina Kokugonza aliyefariki dunia 2018 ikiwa na lengo la kumuenzi bibi yao kwa namna alivyokuwa akiishi na jamii na familia kupenda kwaweka pamoja bila kujali uwezo wao wala itikadi za kidini au za vyama katika suala la kuleta maendeleo.

Mwenyekiti wa Kijiji Rwanda, Majid Ayub, akikabidi zawadi kwa washindi wa pili wa michuano ya BBI CUP timu ya Kitunga-Kyamawa baada ya mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga, Kamachumu mkoani Kagera juzi.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles