25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA STANBIC YAZINDUA TAWI DAR

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


BENKI ya Stanbic Tanzania imefungua tawi jipya lenye huduma zote jijini Dar es Salaam, katika jitihada zinazolenga kutoa huduma bora za kibenki kwa wateja wake.

Tawi hilo jipya la Peninsula linafikisha idadi ya jumla ya matawi nane ya benki hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa tawi hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic, Ken Cockerill, alisema hatua hiyo imefikiwa wakati benki ikifanya jitihada za kusogeza karibu huduma zake kwa wateja wanaozidi kuongezeka.

 “Benki ya Stanbic imewekeza zaidi katika ugunduzi wa huduma zitakazomwezesha mteja kujihudumia kupitia huduma za kibenki mtandaoni na kwa njia ya simu, bado tunatambua umuhimu wa kuzungumza na wateja wetu na kuwapatia huduma mahsusi zinazolingana na mahitaji yao,” alisema.

Alisema uongezwaji wa tawi la Peninsula katika idadi ya matawi ya benki hiyo unadhihirisha uthabiti wa benki hiyo katika kufikia watu wengi na kuzisaidia biashara nyingi zaidi kukua.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, aliipongeza Benki ya Stanbic kwa jitihada zake za kuunga mkono miradi ya miundombinu, kutoa huduma maalumu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati na kwa mwendelezo wake wa kutoa huduma zilizo na ubunifu mkubwa.

Kutokana na hali hiyo, aliiasa sekta ya kibenki kutumia weledi walionao ili kuongeza thamani katika sekta mbalimbali.

Alisema ni lazima wadau mbalimbali wafanye kazi kwa pamoja ili kuongeza nguvu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.

 “Mpango huu madhubuti wa maendeleo ya miundombinu utajenga mazingira rafiki katika uendeshaji wa viwanda na unahitaji mkakati wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.

“Ili kufikia malengo yetu ya kufikia pato la kati, ni lazima kuwepo na njia itakayotuelekeza kwenye mabadiliko ya kiuchumi. Na taasisi za fedha zina nafasi ya kipekee katika kuchangia kwa kiasi kikubwa kuleta mafanikio haya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles