33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Beki Azam FC amcheki Ronaldo Brazil

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

BEKI wa zamani wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, Azam FC, Joackins Atudo, juzi alikuwa kwenye Uwanja wa Nacional de Brasilia nchini Brazil kumshuhudia nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo katika mechi ya Kombe la Dunia waliyocheza dhidi ya Ghana.

Atudo alishuhudia Ureno ikiifunga Ghana mabao 2-1, huku Ronaldo akifunga bao la ushindi kwa timu yake hiyo. Beki huyo aliikacha Azam FC mwaka jana na kujiunga na Tusker ya Kenya, baada ya mkataba wake wa kuwatumikia mabingwa hao kwisha.

Beki huyo wa kati kwa sasa yupo nchini Brazil akiwa na wachezaji wenzake 12 wa kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na kocha mkuu, Mfaransa Adel Amrouche.

Harambee Stars imepewa ofa na Rais wao wa Kenya, Uhuru Kenyatta kukaa siku tatu nchini humo na kushuhudia mechi ya Kundi H kati ya Ghana na Ureno, ili kuwaongezea uzoefu wachezaji wa kikosi hicho na kuwapa hamasa ya siku moja na wao kufuzu kwa fainali hizo, kesho inatarajia kurejea nchini Kenya.

Wachezaji walioelekea huko ni Cliffton Miheso, Francis Kahata, Paul Kiongera, Jerim Onyango, Musa Mohammed, Jacob Keli, Wilson Oburu, Duncan Ochieng, David Owino, Joe Gachoka, James Situma, Wycliffe Kasaya na Atudo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles