27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

‘Becoming’ cha Michelle Obama chaongeza joto urais 2020 Marekani

WASHINGTON,Marekani

KITABU alichokitoa hivi karibuni kilichobeba jina la ‘Becoming’ kimemuingiza tena katika uwanja wa siasa,Michelle Obama ikiwa ni awamu ya pili ambayo imezidisha joto la kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 dhidi ya rais Donald Trump tangu kumalizika ule wa mwaka 2016.

Michelle ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Marekani,Barack Obama, tetesi za yeye kuwania urais mwaka 2020 nchini humo zimeongezeka kutokana na ziara anayoifanya katika miji kumi mikubwa ya kukitangaza kitabu chake hicho.

Mbali na ziara yake hiyo ambayo imemkutanisha na watu wengi akiwamo Meghan Markle katika kikao cha faragha huko jijini London nchini Uingereza, hatua yake ya wiki chache zilizopita kujitokeza hadharani na kuhamasisha watu wasio na vyama  kupiga kura katika uchaguzi  uliofanyika Novemba 4 mwaka huu wa maseneta na magavana ndio unaelezwa kuamsha umma na hata baadhi kujenga hisia kuwa Michelle anajiandaa na urais mwaka 2020.

Inaelezwa kuwa Michelle amekuwa miongoni mwa watu maarufu katika siasa za Marekani, huku kura za maoni zikionyesha ameendelea kuungwa mkono kwa zaidi ya asilimia 60.

Uchambuzi wa kura ya maoni ya  Zogby uliotolewa Mei mwaka huu unapendekeza, Michelle pengine angeanza kutumia fursa ya sasa dhidi ya rais Donald Trump .

Kura ya maoni iliyoendeshwa na Zogby inaonyesha Michelle ana asilimia 48 dhidi  ya asilimia 39 za Rais Trump.

Wakati katika kura ya maoni ya yougov.com iliyofanywa mwezi Aprili mwaka huu inaonyesha chama cha Democrat kinapewa asilimia 90 ya kushinda katika uchaguzi ujao.

Watu wengi ndani ya chama cha Democrat wanapiga kelele za kutaka Michelle agombee urais 2020.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wamebainisha kuwa Obama anamuongezea nguvu  ya kimaadili Michelle ya kuomba kugombea katika uchaguzi ujao.

Duru hizo za kisiasa zimeongeza kwa kusema wakati nchi ikionekana kuwa vipande vipande kuliko wakati mwingine, ile sauti ya kuhamasisha ya Michelle nayo inaelezwa kumpa nguvu ndani ya chama cha Democrat na Marekani kwa ujumla kuwania nafasi hiyo ya juu.

Wanasema ni sauti ile ile ambayo aliitoa wakati akiwa kama mke wa Rais, na wakati ambao alikuwa akijaribu kuondoka kwenye siasa  akitangaza kujikita kwenye masuala ya afya za watoto na lishe pamoja na kusaidia familia za kijeshi.

Michael Starr Hopkins, mwanamikakati wa chama cha Democrat na mkongwe  wa kampeni za mwaka 2008 za Rais Obama anasema; “Michelle anapozungumza haonekani kutoka kwenye historia ya siasa lakini anachozungumza  kina ujumbe halisi na watu wanamwamini sana,”

Katika uchambuzi wao wa nani anayepaswa kuwa mgombea urais, tovuti hiyo iliyojikita katika chambuzi za maoni ya kisayansi kuhusu siasa, uchumi na michezo ya FiveThirtyEight (538) imechambua kuwa huenda kitabu cha Michelle cha ‘Becoming’  kutoka sasa ni sehemu ya kampeni kuelekea 2020.

Zaidi wanasema ni kiashiria kama kuna mtu anajipanga kwa ajili ya kuwania urais. Aidha, wapo wanaosema Michelle anajiona hana sifa za kugombea urais.

Pamoja na kipaji chake cha uongozi alichonacho, haiba na umahiri wa hotuba zake  za kuhamasisha anasema haguswi na siasa.

“Sababu kwa nini sitaki kuwania urais na siwezi kusema kwa Oprah, lakini hisia zangu ni kwamba, kwanza kabisa, unahitaji kazi,” alikaririwa Michelle akisema  katika mkutano wa 39  wa Simmons Leadership.

Hata katika uchambuzi wake Perry Bacon Jr wa  FiveThirtyEight anasema haamini kama Michelle anapanga kuwania urais lakini anasema huwezi kujua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles