27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BAYERN MUNICH WATALIPA KISASI KWA REAL MADRID?

Na BADI MCHOMOLO


UHONDO wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), unatarajia kuendelea wiki hii kwa viwanja viwili kutimua vumbi.

Hii ni hatua ya kwanza ya nusu fainali kabla ya michezo miwili ya marudiano kupigwa wiki ijayo.

Hiki ndicho kipindi ambacho wadau wa soka wanapenda kutumia neno ya mtoto hatumwi dukani kwa kuwa ushindani wa hatua hii ni mkubwa tofauta ni ile iliopita.

SPOTIKIKI leo hii imekufanyia uchambuzi wa michezo hiyo miwili huku ikiamini kuwa mchezo wa Bayern Munich dhidi ya Real Madrid utakuwa wa kisasi.

Bayern vs Real Madrid

Kikubwa ni ubora wa timu pamoja na mifumo ya kocha inaweza kuifanya timu yoyote kuweza kusonga mbele hatua ya fainali.

Madrid wana lengo kubwa la kutaka kuandika historia ya aina yake ambayo haijawahi kuandikwa na timu yoyote katika historia ya michuano hiyo.

Madrid ni klabu ya kwanza kuweza kutwaa taji hilo la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo, haijawahi kutokea, hivyo wanataka kupambana ili wahakikishe wanalichukua tena kwa mara ya tatu mfululizo.

Mbali na Madrid kuingia kwenye historia hiyo ya kuchukua mara mbili mfululizo, lakini kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane akiwa na lengo la kutaka kuweka historia ya aina yake ambayo haijawahi kuwekwa na kocha mwingine.

Mchezo huo utapigwa Jumanne hii, hivyo Bayern Munich watashuka dimbani kulitafuta taji hilo kwa nguvu huku tayari wakiwa wametangazwa kuwa mabingwa wapya kwa mara sita mfululizo huko nchini Ujerumani.

Mbali na kuwa na furaha ya kuwa mabingwa mara sita wa Ligi Kuu nchini Ujerumani, ila kwenye mchezo huo wa kesho watakuwa kwenye kumbukumbu ya kipigo walichokipata msimu uliopita kwenye michuano hiyo.

Msimu uliopita Madrid walionekana kuwa wababe dhidi ya Bayern Munich nyumbani na ugenini.

Mabingwa hao watetezi walipata ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa robo fainali huku Madrid wakiwa ugenini, wakati mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid walishinda mabao 4-2 na kuwa na jumla ya mabao 6-3.

Hiyo ilikuwa kwenye robo fainali, ila kwa sasa wanakutana kwenye mchezo wa nusu fainali, hivyo Bayern wapo kwenye mipango ya kulipa kisasi.

Timu hizo jumla zimekutana mara 20 tangu mwaka 2000, lakini Real Madrid wanaonekana kuongoza kumfunga mpinzani wake, akishinda mara 10 wakati huo Bayern Munich wakishinda mara tisa na wakitoka sare mara moja.

Madrid msimu huu hawakuwa kwenye kiwango kizuri hasa kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania, lakini kwenye hatua hii ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa wanaonekana kuamka na kuonesha makali yao kwa kutaka kutetea ubingwa huo ambao wameuchukua mara mbili mfululizo.

Bayern wao wanataka kuweka historia mpya baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo huku akiwaambia watarajie makubwa. Kauli hiyo aliisema baada ya kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ujerumani.

Hata hivyo kocha huyo amekuwa na historia kubwa ndani ya Bayern Munich kwa kuwa aliweza kuwapa mataji manne ya Ligi Kuu kwa wakati tofauti, hivyo amedai anataka kuendeleza heshima yake ndani ya kikosi hicho hasa kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.

Liverpool vs AS Roma

Huu ni mchezo mwingine wa kulipiza kisasi, mashabiki wa AS Roma dua zao walikuwa wanaomba kwenye hatua hiyo wakutane na Liverpool, sio kutokana na ubora wake, ila ni kutaka kulipa kisasi.

Hii inatokana na AS Roma kutokuwa na historia nzuri kwa wapinzani hao, hivyo walikuwa wanaomba kukutana nao ili walipize kisasi.

Katika historia timu hizo zimekutana mara tano tangu mwaka 1983, hivyo katika mara tano walizokutana Liverpool imeshinda mara mbili, AS Roma wakishinda mara moja na kutoa sare mara mbili.

Hiyo inaweza kuwa sababu ya mashabiki wa AS Roma kuomba wakutane na Liverpool kwa ajili ya kutaka kulipa kisasi.

Mchezo huo wa nusu fainali unatarajiwa kupigwa Jumanne ya wiki ijayo kwenye uwanja wa Anfield kabla ya marudiano Mei 2.

Liverpool ni klabu pekee kwenye michuano hiyo kusalia kwa klabu ambazo zinatoka nchini England, hivyo kesho wanataka kuonesha kuwa walikuwa na sababu ya kubaki kwenye michuano hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles