27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Bayern Munich haikamatiki

 MUNICH, UJERUMANI 

VINARA wa Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, Bayern Munich, wameendeleza wigo wa pointi nne dhidi ya Borussia Dortmund ambapo timu hizo mbili a juu zinakutana kesho katika muendelezo wa mechi za Bundesliga. 

Bayern Munich waliwafunga Eintracht Frankfurt 5-2 mwishoni mwa wiki iliyopita na kuongeza wigo hilo la ponti ambalo awali lilikuwa limepunguzwa hadi moja kufuatia Dortmund kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Wolfsburg. 

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Bayern Munich walikuwa kifua mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Leon Goretzka na Thomas Muller, na dakika moja baada ya kipindi cha pili kuanza, Robert Lewandowski, aliongeza bao la tatu kwa kichwa. 

Hata hivyo, Frankfurt walionyesha uhai kwa kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu kupitia beki Martin Hinteregger aliyetupia mabao yote mawili. 

Lakini ndoto zao zilididimizwa baada ya Alphonso Davies kutumia makosa ya mabeki wa Frankfurt na kufanya scoreboard kusoma 4-2 kabla ya Hinteregger kujifunga akijaribu kuokoa krosi ya Serge Gnabry. 

Frankfurt ambao wamekuwa aking’ang’ana msimu huu wamepoteza mechi tano mfululizo za Bundesliga na hii ni mara ya pili wanafungwa mabao matano na Bayern. 

Kesho, Bayern Munich watataka kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 4-0 na Dortmund nyumbani kwao katika mchezo wa mzunguko wa kwanza. 

Kinachoufanya mtanange wa kesho uwe wa ‘kufa mtu’ na kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka la Ujerumani ni nafasi ya kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu hiyo. 

 Bayern Munich wamekaa kileleni wakiwa na pointi 61, wakati Dortmund wanashika nafasi ya pili kwa pengo la pointi nne tu, ambazo zitapungua na kubaki moja endapo watashinda mechi ya kesho. 

Je, Bayern watakubali kufungwa ili wapumuliwe na Dortmund kwa pointi moja? Dortmund nao watakubali kufungwa wakati wanafahamu wataongeza pengo na kufikia pointi saba?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles