Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) limesema Vyuo Vikuu vingi vipo hatarini kufungwa kwani Serikali imeshindwa kulipa madeni inayodaiwa.
Hali hiyo inavipa ugumu wa kujiendesha huku wanafunzi nao wakikosa mikopo.
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.
“Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 60 na Vyuo Vikuu, tunamtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndarichako atoe kauli ya serikali ndani ya siku saba juu ya jambo hili.
Walimu wakuu wa vyuo wanaogopa kueleza ukweli kwa hofu ya kutumbuliwa, Profesa Ndalichako akishindwa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aseme, naye kama anaogopa kutumbuliwa basi Rais Dk John Magufuli atueleze, tupo pabaya elimu inachezewa, ” amesema Katambi