Batuli atamani watoto mapacha

0
1085

YobneshYusufbatuliNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM
MSANII wa filamu za kibongo, Yobnesh Yossuf ‘Batuli’, amesema anatamani kupata watoto mapacha wa kike katika maisha yake.
Akizungumza juzi alipotembelea ofisi za gazeti hili, mrembo huyo mwenye watoto wawili wa kiume, alisema moja ya mipango yake ni kupata mtoto mwingine wa kike, tena ikiwezekana mapacha.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kupata watoto wa kiume wawili, lakini bado nina mpango wa kuongeza wengine wa kike na nitafurahi nikipata mapacha, lakini nikishindwa kabisa nitatumia njia kama wanazofanya wazungu za kuasili,” alisema.
Batuli alianza kujulikana katika tasnia ya filamu baada ya kucheza filamu ya ‘Fake Smile’, ambayo alishirikishwa na marehemu Steven Kanumba, huku akiwa amecheza filamu nyingine mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here