32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bashiru: Mambo mawili ambayo mwalimu hakuyatendea haki

Anna Potinus

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally ameyataja mambo mawili muhimu ambayo Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere alikiri kutokuyatendea haki na hivyo kuwataka viongozi wanaokuja kuyafanyia kazi.

Dk. Bashiru amewataka Watanzania kuacha kumuenzi na kumkumbuka Mwalimu Nyerere kama mtakatifu kwasababu yeye ni binadamu na kwamba moja ya sifa yake kubwa ilikuwa ni kukiri makosa.

Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza katika kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Ninataka nizungumzie mambo ambayo mwalimu aliyaona kama makosa na leo tunamzungua kama vile hajawahi kukosea ni mtu ambaye alikuwa anakiri makosa yake kwahiyo tusimuenzi na kumkumbuka kama mtakatifu kwasababu yeye ni binadamu na moja ya sifa yake kubwa ilikuwa ni kukiri makosa,”.

“Katika mambo ambayo mwalimu alikiri na kataka tusiyarudie ni pamoja na hakufanya vizuri kuimarisha serikali za mitaa pia hakufanya vizuri katika eneo la ushirika kwa maana ya kwamba kuwa na vyombo vya kutetea wanyonge na kulinda jasho la wanyonge,”.

“Tuko katika mchakato wa serikali za mitaa sisikii vishindo kama vvile vya kutafura rais na mbunge lakini kumbe wale viongozi wa serikali za mitaa ndio tunaoishi nao na kuna wengine hawajui kama leo tumeshaanza kujiandikisha,” amesema Dk. Bashiru.

Amewataka Watanzania  kutumiana ujumbe kukumbushana kwamba wana jukumu la kujiandikisha katika maeneo wanayoishi ili wachague viongozi ambao watawasaidia kutatua matatizo yao ya kila siku na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi baba wa taifa katika eneo ambalo yeye mwenyewe alikiri kuwa hakufanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles