31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali watakiwa kutumia fursa ya Elimu na mikopo kutoka Benki

Derick Milton

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa kutumia vyema elimu ya biashara ambayo wamekuwa wakipewa na taasisi za kifedha hapa nchini ikiwemo benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonyesho ya viwanda vidogo (SIDO) kitaifa yanayofanyikia mkoani Singida, ambapo amewataka kutumia fursa hiyo katika kuboresha biashara zao.

“Nimekutana na taasisi mbalimbali za kifedha, ikiwemo NBC, na wote hawa wanatoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali wote, niwasihi tumieni vizuri fursa hii katika kuboresha biashara zetu,” amesema Majaliwa.

Akiongea na Mtanzania Digital Meneja wa NBC Mkoa wa Singida Thomas Lijaji alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa elimu pamoja na mikopo ili waweze kukuza biashara zao.

“Tunajua endapo hawa wajasiriamali ambao tunawapa elimu na mikopo watakuza biashara zao, na endapo zitakuwa tutakuwa na wateja walioimarika zaidi na wenye uwezo wa kukopa mikopo mikubwa zaidi,” amesema Lijaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles