25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Basata yaipa kibali cha muda Miss Tanzania

miss-tzJULIET MORI NA LETICIA BWIRE (TUDARCO)

MASHINDANO ya urembo ya Miss Tanzania yaliyofungiwa kwa muda wa miaka miwili yamepata ahueni baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuipa kibali cha muda kampuni inayoendesha shindano hilo, International Agency Limited (LINO).

Basata imetoa kibali hicho cha muda kisichozidi miezi minne kwa ajili ya maandalizi ya awali, ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote husika ili kuboresha na kurudisha heshima ya shindano la Miss Tanzania.

Shindano la Miss Tanzania lilifungiwa Desemba 22 mwaka jana kwa muda wa miaka miwili na kuagiza kampuni hiyo kujipanga upya na kurekebisha kasoro zilizokuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, aliwaambia waandishi wa habari jana katika ukumbi wa baraza hilo uliopo Ilala, jijini Dar es Salaam kwamba kulikuwa na mapungufu ya mawakala wanaondesha shindano hilo.

Alisema mawakala waliopo hawakufuata kanuni na taratibu za uendeshaji wa shindano hilo, ikiwemo mikataba ya washiriki na pia wengine hawakuwa na vibali vya kuendesha shughuli hiyo.

“Tuna imani kwamba kampuni ya Lino itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa matukio ya sanaa nchini na haitarudia makosa yatakayolisababishia shindano hilo kushuka viwango,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles