24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la mawaziri wa EAC laidhinisha DR Congo kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Nairobi,Kenya

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iko hatua moja karibu na kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya baraza la mawaziri la eneo hilo kupitisha kujiunga kwake

Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walipiga kura ya kuunga mkono DRC baada ya kumalizika kwa mazungumzo makali jijini Nairobi. DRC inaonekana kama soko muhimu kwa eneo hilo kutokana na maliasili yake kubwa.

Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sasa inasubiri tu idhini ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao watakutana baada ya wiki chache.

Kuidhinishwa kwa baraza la mawaziri ni hatua kubwa kwa DRC ambayo iliomba uanachama mwaka 2019. Inakuja baada ya kumalizika kwa majadiliano ambayo yalilenga kuanisha sera za nchi hiyo za kijamii na kiuchumi na zile za EAC na utayari wake na uwezo wake wa kuzingatia sheria za EAC.

Hii ni pamoja na hadhi ya mfumo wa kodi wa DRC na sheria za kimataifa. Kujumuishwa kwa soko la DRC la karibu watu milioni 90 kutapanua soko la EAC kufikia zaidi ya watu milioni 300 na kufungua umoja huo kwa uchumi wa DRC ambao una utajiri mkubwa wa maliasili.

Kukubaliwa kwa DRC kutaifanya kuwa mwanachama wa saba wa kanda hiyo inayojumuisha Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles