Na​ Renatha Kipaka, Bukoba
Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba MkÂoani Kagera limeonya watendaji wanaosabaÂbisha upotevu wa fedÂha za​ makusanyo ya ndani kwa kutoyafikiÂsha benki.
Hayo yalibainishwa juzi kwenye kikao cha kupoÂkea na kujadili taarÂifa ya mkaguzi na mtÂhibiti wa​ hesabu za serikali ( CAG)wakaÂti wa​ majadiliano ya maoni ya Baraza hilo.
Akitoa maoni ya taarÂifa hiyo Diwani wa Kata ya​ Bakoba ShambÂani Rashid alisema uÂkusanyaji wa mapato unafanywa na​ watendÂaji ambapo kwa kipinÂdi cha mwaka 2019/20Â,20/21 kiasi cha Sh Âmilini 3.5 haikufishwa benki
“Kuna shilingi MilioÂni tatu pointi tano tunayoiona hapa haikufikishwa benki na unaonyesha ilikusanywa kwa njia ya POS hili litolewe onyo Kali ili kurekebisha makoÂsa yalisijirudie kipinÂdi kingine,”alisema Rashid.
Diwani wa kata ya Bilele, Theofiki Salum alÂisema ilikufanikiwa kwenye suala la fedÂha kuwepo na ushirikÂiano katika kusimamia mapato​ lazima kuuÂnda kamati za fedha, elimu na nidhamu.
“Watumishi watambue sio​ lazima viongozi wa juu wafike kubaÂini madhaifu bali kuÂtengeneza weledi na kupata hati safi na fedha zionekane kupaÂnua miradi,”alisema Salumu
Awali, akisoma taarifa mbele ya Baraza hiÂlo, iliyopokelewa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutoka kwa (CAG) Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Profesa Faustine Kamzora aliÂsema, licha ya HalmaÂshauri sita ndani ya mkoa huo kuÂpata hati zinazolidhÂisha
Prof. Kamzora alisema ManiÂspaa ya Bukoba kwa mwaka 2019/20,20/21 hakuweza kupeleka kiaÂsi cha Sh.milioni 25Â6.4kwenye miradi ya Maendeleo
Aliongeza kuwa, upanÂde wa fedha ya akina mama na vijana ambaÂyo ni​ Sh.milini 148Â.5​ haikuweza​ kufanyÂiwa ufuatiliaji kuliÂngana na muda wake kuisha.