26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari Dar kuondoa tatizo la meli kukaa muda mrefu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Bandari ya Dar es Salaam imesema ipo kwenye hatua nzuri ya utekelezaji ujenzi wa kituo kipya cha majumuisho cha meli kubwa za mafuta kitakachoondoa changamoto ya meli hizo kukaa muda mrefu na kupunguza gharama.

Hayo ameyabainishwa leo Januari 14,2024, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Bandari hiyo Mrisho Mrisho, ailpofanya oparesheni za kibandari kuanzia gati namba 0 hadi 11.

Amesema gati namba 0 ni maalumu kwa magari ambapo uwezo wa kuhifadhi magari 250,000 hadi 300,000 kwa mwaka.

Ameleza kuwa katika eneo la namba 0, linahudumia meli za mwambao Zanzibar na Comoro, huku mifumo ya ulinzi ikiimarishwa kukiwa na jumla ya kamera 470 zinafanya kazi katika maeneo mbalimbali ya bandari hiyo.

“Kwa sasa hatuna tanki za kuhifadhi mafuta katika bandari yetu ambapo mafuta yakifika yanaenda moja kwa moja kwenye maghara ya wadau lakini Serikali pia ipo kwenye mazungumzo na Jeshi la Maji (NAVY) upande wa pili wa bandari kujenga gate no 5 kwa ajili ya tanki za mafuta ,”amesema Mrisho.

Amesema gati namba 1 hadi 4 ni maalumu kwaajili ya mizigo mchanganyiko na miradi ya kitaifa ikiwamo SGR na Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Kuhusu gati no 5,6,7 amesema ni maalumu kuhudumia shehena ya makontena 1800 na kupakia 13000.

Amesema moja ya vitu vinaongeza ufanisi ni kuhudumia shehena za makotena kwa kupakua na kushusha.

Aidha amesema TPA ina mitambo maalumu mipya ambayo itakuwa inaendeshwa na umeme na inafanyakazi masaa 22 hadi 24 mbayi inatoka kampuni ya Liebherr hivyo mkandarasi yupo kazini kufanikisha upatikanaji WA umeme kwa saa 24.

“Chanzo cha umeme wa mitambo hiyo ni Ilala na Temeke ili kusiwe na shida ya kukatikakati kwa umeme tunatarajia kuwa na kv 33 za umeme katika gati namba 5,6,7 kwa ajili ya mitambo mipya,” amesema.

Mrisho amesema gati namba 11 ni maalumu kwa ajili ya meli kuhudumia makasha au kontena, linahudumia zaidi ya 1,200,000 kwa mwaka.

Ameeleza kuwa Kurasini Oil Jet ni moja kati ya maeneo mawili yanayohudumia shehena ya mafuta.

Amesema kuongeza gati maalum kwa meli za Barrick kutaondoa changamoto wakati wa mvua za El-Nino.

Aidha Mrisho amesema Januari 16, 2024 wanatarajia kupokea meli kubwa ya watalii yenye mita 294, hivyo ni kuongeza miundombinu itasaidia ufanisi wa kuhudumia meli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles