27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Baba wa mwigizaji afariki Dar

ZittaNA SUZANA MAKORONGO (RCT)

MKALI wa filamu ya ‘Gundu’, Zitta Matembo maarufu kwa jina la Da Zitta, amefiwa na baba yake mzazi, Fidelis Hokororo Matembo, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mzee Matembo ambaye alikuwa mwanajeshi mstaafu kikosi cha 511KJ Gongo la Mboto, alianza kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo tangu mwishoni mwa mwaka jana, alilazwa katika Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi, kisha alihamishiwa Muhimbili kitengo cha moyo ambapo aliendelea na matibabu.

“Alipoletwa Muhimbili aliendelea na matibabu hadi Jumatatu hali ikawa mbaya akaingizwa chumba cha watu mahututi (ICU) na asubuhi ya jana alifariki dunia, tunatarajia kumsafirisha leo kwenda Masasi mkoani Lindi kwa ajili ya mazishi yake,” alisema Zitta.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles