27 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Azam FC yamtesa Pluijm

IMG_2749MSHAMU NGOJWIKE, MORO NA RODRICK NGOWI, MWANZA

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm, amesema Azam FC ndio timu inayomuumiza kichwa kwa sasa kutokana na wote kuwa na pointi 15 kileleni.

Pluijm alitoa kauli hiyo juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro alipoichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 na kuvunja uteja wa Yanga kutoifunga Mtibwa Sugar mkoani humo ndani ya miaka mitano.

“Lakini kwa sasa nazifikiria mechi zijazo, tunacheza na African Sports na baadaye Azam FC ambayo ndiyo mechi ninayoifikiria ili niweze kujihakikishia kukaa kileleni kwa amani,” alisema.

Mholanzi huyo alisema anafahamu ugumu uliopo kwa kila mchezo hasa mechi za mikoani lakini anaifikiria zaidi Azam ambayo imekuwa ikikabana naye koo kileleni mwa msimamo zote zikiwa hazijafungwa mechi hata moja.

Azam na Yanga zimekuwa na upinzani mkubwa kwa siku hivi karibuni kwenye mechi zao, mara ya mwisho zilipokutana msimu uliopita Azam ilishinda mabao 2-1 na wa kwanza ukiisha kwa sare ya 2-2.
Akizungumzia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Pluijm amesema licha ya kuwafunga, wameonyesha kiwango cha hali ya juu tofauti na walivyofikiria.
“Ni timu nzuri sana, sikufikiria kuwa kuna timu bora kiasi hiki, ila hawa wanachokosa kuwa na wachezaji wa kigeni ambao wataweza kubadili
mchezo katika mechi ngumu,” alisema.

Naye Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, aliitupia mzigo wa lawama safu yake ya ulinzi kwa kufanya makosa ya kijinga yaliyowagharimu na kupoteza mchezo huo.

“Ni walinzi ambao wameniangusha, mabao yote yalitokana na uzembe wa mabeki, lakini mchezo huu tulikuwa na asilimia nyingi tu za kushinda,” alisema.

 

Toto African yashikwa Kirumba

Wakati huo huo, timu ya Toto African imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Kirumba, jijini Mwanza.

Mbeya City ndio iliyoanza kufunga bao dakika 12 likifungwa kwa mpira wa adhabu ndogo na John Kabanda uliomshinda kipa wa Toto, Musa Mohamed, ambaye alianza kuzomewa na wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa Simba.

Toto African iliamka kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 76 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Edward Christopher.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles