KLABU ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, imekabidhiwa Sh milioni 5 ya Goli la Mama kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kutokana na ushindi wake bao 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wengine walionyakua zawadi hiyo ya Goli la Mama ni Yanga SC, walioibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya wageni wao Vitalo ya nchini Burundi, ambapo kwa matokeo hayo timu hiyo ya Tanzania ilikabidhiwa Sh milioni 20 kutoka kwa Rais Samia.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Dumbaro, alimshukuru Rais Samia kwa kuamua kujitosa kusaidia ukuaji wa michezo ukiwemo mpira wa miguu kwa kutoa zawadi za magoli ya ushindi kwa timu za Tanzania zinazocheza mashindano ya kimataifa.