29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Azam FC bila Cioaba, Dube kuishukia Biashara leo

Asha Kigundula -Dar es salaam                                      

LIGI Kuu Tanzania Bara, inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa, ambapo Azam itakuwa ugenini Uwanja wa Karume mkoani Mara kuumana na wenyeji wao Biashara United. 

Azam itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wake uliopita ikiwa nyumbani, baada ya kuchapwa bao 1-0 na Yanga, kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Majanga kama hayo pia yaliikuta Biashara ambayo katika mchezo wake uliopita ilitandikwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita , Azam ilishinda mabao 2-1, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Huo ulikuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza, lakini ziliporudiana Uwanja wa Karume, dakika 90 zilikamikika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo, Azam itashuka uwanjani bila ya uwepo wa mshambuliaji wake tegemeo, Prince Dube, ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya mkono.

Dube alipata jeraha hilo wakati wa mchezo dhidi ya Yanga na kulazimika kutolewa nje dakika ya 23.

Azam pia  haitakuwa na kocha mkuu, baada ya aliyekuwa akihudumu nafasi hiyo Mromania, Aristica Cioaba, kufutwa kazi baada ya  kipigo cha Yanga.

Badala yake benchi la ufundi la  timu hiyo litaongozwa na Vivian Bahati, ambaye anakaimu nafasi ya Cioaba.                                     

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 25, ikishinda michezo nane, sare moja na kuchapwa mara tatu.

Biashara kwa upande mwingine, ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 18, baada ya kucheza michezo 12,ikishinda mitano, sare tatu na kuchapwa mara nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles