26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Azaki, Sekta Binafsi na Umma kushirikiana kuleta maendeleo kwa jamii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), limeandaa mpango kazi utakaosaidia AZAKi kujikwamua kiuchumi kutokana na ushirikano utakaozikutanisha pamoja na Sekta Binafsi katika utekelezaji wa shughuli zao mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Hayo yamebainishwa na Afisa Oparesheni na rasilimali watu wa FCS, Karin Mbaga Rupia, wakati wa warsha maalum iliyofanyika jijini Arusha katika maadhimisho ya Wiki ya AZAKi inayoendelea Jijini humo.

Karin amesema kuwa mpango kazi huo utakuwa mbadala wa AZAKi kujipatia fedha za kutekeleza miradi yake katika kuisaidia jamii, na kuboresha uhusiano mzuri kati ya AZAKi na Sekta Binafsi na Mashirika ya umma.

“Kwa zaidi ya miaka ishirini ya uzoefu wetu wakufanya kazi na Asasi ndogondogo za kiraia kote nchini tumekuwa tukitoa ruzuku, kwa Asasi hizo, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele uwezo wetu wa kifedha unazidi kupungua kutokana na mataifa ya nje tuliyokuwa tukiyategemea kwa msadaa wa kifedha kupunguza nguvu kutokana na athari za kiuchumi zinazoikumba Dunia. Hivyo tumebaini njia mbadala ya kujiimarisha kiuchumi ni kufanya kazi kwa kushirikiana na Sekta Binafsi na mashirika ya umma,” amesema Karin.

Kwa upande wake mwezeshaji wa warsha hiyo, Sara Teri ameeleza kuwa mpango kazi huo utazipa fursa AZAKi, Sekta Binafsi na Umma, kushirikiana kuleta maendeleo kwenye jamii.

Ameongeza kuwa hiyo ni hatua muhimu kwa AZAKI na Sekta Binafsi, nakwamba itasaidia kutatua athari za kimazingira na changamoto za maendeleo katika jamii.

Naye mdau wa AZAKi ambaye pia ni Mbunge mstaafu, Janeth Mbene, amefurahishwa na mchakato huo na kusema kuwa ili Taifa lipige hatua zaidi kimaendeleo na kufanikisha Dira ya maendeleo ya Taifa 2050 hakuna budi Asasi za kiraia, Sekta Binafsi na Umma kuwa kitu kimoja katika kila hatua kwa maslahi mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles