Canberra, Australia
Nchi ya Australia inatarajiwa kufunga ubalozi wake nchini Afghanistan wiki hiikufuatiwa machafuko yanayoendelea nchini humo.
Taarifa iyo iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison, amesema ubalozi huo utafungwa kutokana na mazingira ya usalama yasiyo na uhakika mjini Kabul huku wanajeshi wa kigeni wakiwa wanajiandaa kuondoka nchini humo.
Pia Waziri Morrison ameongezea na kusema ubalozi huo utafungwa mnamo Mei 28 huku Marekani imeanza kuondoa rasmi wanajeshi wake Afghanistan, hali inayozuwa hofu ya kukosekana usalama kutokana na kitisho cha kundi a Taliban.
Serikali ya Afghanitan pamoja na vikosi vyake vya usalama bado ni dhaifu licha ya miongo miwili ya usaidizi wa kigeni.
Wanajeshi wengi wa Kimarekani wanatarajiwa kuondoka mnamo Septemba 11, ikiwa ni miaka 20 tangu shambulio la al-Qaeda mjini New York lilopelekea Marekani kuivamia Afghanistan.