28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

AUBAMEYANG AMPIGIA DEBE WIZKID

LONDON, ENGLAND


NYOTA wa soka kutoka klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, ameonekana kumpigia debe mkali wa muziki wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, Wizkid, baada ya kuvaa jezi yenye nembo yake ya Starboy.

Hivi karibuni msanii huyo alitangaza kufungua duka lake la nguo huko jijini Los Angeles nchini Marekani na kudai kuwa atafanya hivyo sehemu mbalimbali duniani ili aweze kuwafikia mashabiki zake.

Katika maduka hayo kutakuwa na baadhi ya nguo zenye nembo yake ya Starboy, ambazo kwa sasa zipo mitaani, lakini kupitia ukurasa wa Instagram wa Aubameyang raia wa nchini Gabon, aliposti picha akiwa amevaa jezi yenye nembo ya Starboy na kudai anamshukuru msanii huyo kwa kumpa jezi hiyo.

Mbali na mchezaji huyo kushukuru, lakini alikwenda mbali zaidi na kuwataka mashabiki zake kwenye mtandao huo wa Instagram wafuate linki ambayo aliiweka kwa wale ambao wanataka jezi hizo za Wizkid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles