25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Athari za ‘mask’ zatajwa, hawa ndiyo wanaotakiwa kuvaa…

Mwandishi Wetu

Imeelezwa kuwa si kila mtu anatakiwa kuvaa kifaa cha kuziba uso ‘mask’ (barakoa) ili kujikinga na homa inayosababishwa na virusi vya corona.

Akitoa maelekezo kuhusu watu wanaotakiwa kuvaa mask, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa Mlipuko, Dk. Janeth Mghaba amesema kifaa hicho kinavaliwa si zaidi ya saa nne tu na mtu ambaye tayari ana maambukizi kusudi asimuambukize mwingine.

Amesema hiyo ni kwa sababu siyo rahisi mtu akakohoa aidha kwa kutumia kiwiko au mkono atakuwa na maji maji na mara nyingi ataweza kumuambukiza mwenzie.

“Kwa hiyo yule ambaye ni mgonjwa tu, tunasema kwamba ukijisikia dalili za kukohoa basi wewe vaa mask yako nenda kwenye kituo cha afya karibu au hospitali.

“Mask pia zinaweza kuvaliwa kwenye sehemu za msongamano au sehemu zenye watu wengi lakini kwa sababu tayari serikali imeshapiga marufuku hii misongamano, hatutegemei kukuona wewe unavaa mask unapita sehemu ambako hakuna msongamano na wewe ni mzima huna maambukizi,” amesema.

Aidha, Dk. Mghaba amebainisha kuwa kuna hatari kubwa ya kuvaa mask kwa sababu watu wengi bado hawajawahi kuuzingatia uvaaji wake.

“Mask hizi zinatakiwa kuvaliwa kila baada ya saa nne na kuzibadilisha, usipokuwa na hii tabia ya kuzibadilisha ukakaa nayo siku nzima kwako wewe ni hatari, itakuletea maambukizi mengine zaidi. Kwa hiyo tunashauri matumizi haya ya uvaaji mask yawe yanatumika kwa usahihi,” amesema.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles