25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Fisi ajeruhi walinzi mgodi wa Mwadui

Damian Masyenene, Shinyanga

Walinzi wawili kampuni ya Zenith wamejeruhiwa na fisi wakiwa doria katika mgodi wa Almasi wa Williamson Mwadui mkoani Shinyanga.

Walinzi hao Geofrey Zablon (23) na Modester John (30) walivamiwa na fisi huyo Machi 16, mwaka huu saa 5:03 usiku wakiwa doria na wenzao watano katika mtaa wa Line Polisi ndani ya mgodi wa huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba Zablon alijeruhiwa mkono wa kushoto na mwenzake Modester alijeruhiwa paja la mguu wa kulia.

“Fisi huyo alikimbia mara baada ya walinzi wenzao kumshambulia kwa marungu, majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mgodi wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles