27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

ATCL yastisha safari za India

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesitisha safari zake za ndege kati ya Dar as Salaam na Mumbai (India ) kuanzia Mei 4, mwaka huu hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine ya kurudisha safari hizo.

Hatua hiyo ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini India. Kwa sasa India inakabiliwa na janga kubwa la virusi vya corona.

Hospitali zimelemewa kwa kuwa na wagonjwa wengi na ripoti za watu kufariki mitaani zikiongezeka.

Mataifa ya Afrika yanategemea kupata chanjo kutoka India kwa kutumiwa mpango wa Covax. Ingawa ongezeko la maambukizi limesababishwa kupiga marufuku usafirishaji wa chanjo hizo na kuangazia watu wake kwanza.

Malawi ilipiga marufuku pia wasafiri wanaotoka India, pamoja na Bangladesh, Brazil na Pakistan kutokana kusambaa kwa virusi vya corona katika mataifa hayo.

Si Tanzania pekee upande wa Afrika Mashariki iliyositisha safari za ndege kwenda nchini India.

Kenya imesitisha kwa muda safari za ndege za abiria wanaotoka India. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya Corona nchini India. Kagwe alisema ‘ hali nchini India imekuwa mbaya sana…. Na kulazimu kuzuiwa kwa safari za ndege kwa siku 14 zijazo.

Uganda nayo ilipiga marufuku safari zote za ndege kutoka India kuanzia Mei 1, mwaka huu ili kuzuia wimbi jingine la janga la corona nchini humo .

Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng alisema serikali ilichukua hatua mbali mbali ili kuzuia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivyo .

Hata hivyo kuna safari kutoka India ambazo Uganda ilisema hazitaathiriwa na marufuku hiyo na ni pamoja na;

Nchi nyingine zilizopiga marufuku safari za ndege India ni pamoja na Canada, falme za kiarabu na Uingereza -marufuku zilizoanza kutekelezwa jumamosi iliyopita lakini hazitathiri ndege za kubeba mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles