24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Askari wanahitaji mbinu za mara kwa mara kukabiliana na uhalifu wa kimtandao-Dk. Yonazi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari, Dk. Jimmy Yonazi amesema uhalifu wa kimtandao ni mpana na kila siku teknolojia inakuwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kila mara Jeshi la Polisi linawajengea uwezo askari wake ili kwenda na ulimwengu wa kidijitali.

Amesema Serikali imechukua hatua kwa kutunga Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka  2015 ili kuweza kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa ukishika kasi.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 25,2022 jijini hapa wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wapelelezi pamoja na maaskari wa chumba cha mashtaka wa Tanzania na Zanzibar lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uhalifu wa Mtandao.

Katibu Mkuu huyo  amesema uhalifu wa kimtandao ni mpana na kila siku teknolojia inakuwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kila mara Jeshi la Polisi linawajengea uwezo askari wake ili kwenda na ulimwengu wa kidijitali.

Amesema Serikali imechukua hatua kwa kutunga Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka  2015 ili kuweza  kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa ukishika kasi.

Aidha,amesema Serikali itahakikisha  inaboresha ushirikiano na mataifa ya nje katika utendaji kazi kuhusu suala zima la ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kimtandao

“Kama serikali tutaendelea kufanyia kazi ya mashirikiano baina ya nchi yetu nan chi nyingine katika kuhakikisha tunaimarisha masuala ya mawasiliano ya Tehama  ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao,” amesema Dk. Yonazi.

Naye, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DCI Camillius Wambura amesema mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kutokana na mbinu walizopata ili kukabiliana na uhalifu wa kimtndao kwani maarifa yatawasaidia katika kubadilishana taarifa.

Mkurugenzi huyo wa Mashtaka nchini amewataka wapelelezi  hao pamoja na askari kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi wao  kwani tabia za wachache zimekuwa zikiharibu taswira ya Jeshi jambo ambalo si jema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles