25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Askari JWTZ akamatwa na kilo 20 za mirungi

Na BEATRICE MOSSES, BABAT


 

JESHI la Polisi mkoani Manyara linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha  Monduli mkoani Arusha,   MT 12014 Abdul Ally (25) kwa kukutwa na mirungi kilo 20.

Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, alisema mtuhumiwa  alikamatwa Novemba 12, mwaka huu   jioni.

“Novemba 12 mwaka huu katika eneo la Minjingu Kata ya Nkaiti Tarafa ya Mbugwe, askari wakiwa katika upekuzi wa magari na ufuatiliaji wa taarifa, wakati wanaisimamisha gari   T543 DHJ aina ya Alteza ikitokea Makuyuni –  Arusha katika kizuizi cha mabasi Minjingu walitilia shaka gari hilo.

 

“Ghafla gari hilo lilibadilisha mwelekeo kurudi nyuma kuelekea Arusha na ndipo askari hao walipotilia shaka na   kuifukuza na  kuikamata maeneo ya Nanja ikiwa inaendeshwa na dereva    askari wa JWTZ Monduli Arusha,”  alieleza Kamanda Senga.

 

Senga alisema kwamba baada ya kuipekua gari hiyo kulipatikana bunda 60 za   mirungi (kilo 20). Mirungi hiyo ilikuwa imehifadhiwa kwenye buti la gari hilo.

 

“Mbinu iliyotumika ni kuficha mirungi kwenye buti la gari ili kujipatia kipato kwa njia isiyo halali. Mtuhumiwa amekamtwa kwa mahojiano kubaini mahali alipoitoa na mtandao wake unaendelea,”alisema.

Alisema wakati mtuhumiwa anakamatwa mwenzake alishuka kwenye gari na kutoroka.

Katika tukio jingine, jeshi hilo linawashikilia Alex Lauriant (27) na Humphrey Charles (28), wote wakulima wakazi wa Dareda wakiwa na   bangi misokoto 200 (gramu 572).

 

Watuhumiwa walikamatwa kwa pamoja kwenye makazi ya Alex Laurent wakiwa kwenye harakati za kusokota bangi hiyo ambayo ilihifadhiwa kwenye mfuko wa plastiki maarufu ‘rambo’.

Kamanda Senga, alisema katika tukio jingine  Novemba 10, mwaka huu jioni maeneo ya Wang’waray, Judith Godfrey Uromi (32) mkazi wa Wang’waray ambaye ni mke wa mkufunzi wa Chuo cha Veta Mkoa wa Manyara,  aligundulika akiwa amefariki dunia chumbani kwake baada ya kujinyonga   kwa kutumia khanga aliyoifunga juu dirishani.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles