25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Asas kusomesha watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu

Raymond Minja, Iringa



Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Asas  ameahidi kuwalipia ada kwa miaka minne wanafunzi 10 wanaotoka katika  mazingira magumu wanaosoma kwenye shule ya sekondari ya Bread of Life iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.

Asas ambaye amejinasibu kuwa ni mdau wa maendeleo ya elimu mkoani hapa amesema hayo katika mahafali ya shule hiyo na kuongeza kuwa nia ni kumpunguzia mzigo kwa kuchukua wanafunzi na  kuwalipia ada kwa miaka minne kila mmoja kama juhudi za kuendelea kuchangia elimu mkoani hapa.

“Mzigo mkubwa alio nao mkurugenzi wa shule hii ni mkubwa mno hivyo hana budi kushikwa mkono kwani kila kukicha nimekuwa nikimuona akihangaika kuwasaidia na kuwajali  watoto yatima na  wanaotoka katika mazingira magumu.

“Huyu bwana ni mtu mweye roho ya aina yake sijawahi  kuona mtu mwenye roho ya pekee kama huyu, yaani amekuwa akihangaika huku na huko kuhakikisha hawa watoto hawa wanapata elimu nzuri kama wanavyopata watoto wake,” amesema.

Aidha, Asas amesema ni watu wachache sana wenye moyo kama mchungaji huyo kwani ni wachache sana wanaoamua kurudisha kile kidogo walichobarikiwa kwa watu wasio na uhitaji huku akiahidi kuendele kushirikiana na shule hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo .

Hata hivyo, Asas aliwataka wanafunzi waliomaliza kidato ha nne waende kuwa mabalozi wazuri  wa shule hiyo na wakailinde nidhamu na heshima waliyopata katika shule hiyo ili waweze kufikia malengo waliyokusudia na kuja kuwasaidi wengine wakiwamo wazazi na walezi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles