28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Arusha DC yataja sababu za kutofikia malengo ya ukusanyaji mapato

Na Janeth Mushi, Arusha

Halmashauri ya Arusha imetaja sababu zilizochangia kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2020/21,ikiwa ni pamoja na kokosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa wafanyabishara na kuyumba kwa bishara ya utalii.

Hayo yamesemwa Januari 29, na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Saad Mtambale, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.

Amesema halmashauri hiyo ilijiwekea makisio ya makusanyo ya Sh billioni 59.188 ila hadi Desemba 31 mwaka jana ilikuwa imekusanya zaidi ya Sh bilioni 21.837.

Ametaja sababu hizo ni kukosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa baadhi ya wafanyabiashara na kuwa bila kusukumana wengi wao hawatoi kodi ambapo wamejipanga kama watendaji kutembelea maeneo mbalimbali na kuhakikisha kila anayepaswa kulipa kodi analipa na kwa kiwango kinachotakiwa.

Amesema changamoto nyingine ni kushuka kwa biashara ya utalii ambapo amesema kuwa uchumi wa Arusha unategemea  sana utalii na kutokana na janga la corona lililokumba dunia hali ya utalii bado haijawa nzuri hivyo kuchangia kushuka mapato.

“Watalii wanapokuja kwa wingi biashara nyingi zinachangamka  ushuru wa huduma tupata hapo na ushuru huo ni sehemu ya mapato hivyo tumekutana na changamoto hizi  lakini kuna jitihada mbalimbali  tunaendelea nazo kama watendaji na tutafikia malengo tuliyojiwekea,”amesema Mkurugenzi

Amesema kutokana na sababu hizo wamebuni vyanzo vingine vya mapato ikiwemo shule ya mchepuo wa kingereza ambayo imeshaanza kupokea wanafunzi,urasimishaji ardhi ambapo kwenye kijiji cha Kiserian kilichopo kata ya Mlangarini, hadi Januari 25, 2021 viwanja zaidi ya 3,000 vilitambuliwa na kupimwa ambapo katika mradi huo watapata zaidi ya Sh milioni 400.

Ametaja mkakati mwingine ni kuja na wazo la kuanzisha kituo cha Radio ambacho kitawasaidia kujitangaza na kuondoa changamoto ya wakazi wa halmashauri hiyo.

“Kuna wafanyabiashara wengi waliopo eneo la mita 200 upande wa halmashauri yetu lakini kwa kutokuifahamu halmashauri hiyo wanaenda kulipa kodi halmashauri ya Jiji la Arusha na ili tuweze kujitangaza tumeona tuanzishe radio yetu na tayari tumeshaanza kulifanyia kazi,”ameongeza Mkurugenzi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles