32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

ARSENAL WAANZA KUMPONDA SANCHEZ

LONDON, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Arsenal kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Crystal Palace, mashabiki wa timu hiyo waanza kumshambulia Alexis Sanchez.

Arsenal walikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani wa Emirates, hivyo waliweza kutembeza kichapo kwa Palace bila ya kuwa na mshambuliaji wao Sanchez.

Sanchez hakuwepo kwenye mchezo huo kwa madai kwamba anakamilisha uhamisho wake na klabu ya Manchester United.

Mabao ya Arsenal yaliwekwa wavuni na nyota wao, Nacho Monreal katika dakika ya sita, Alex Iwobi dakika ya 10, Laurent Koscielny dakika ya 13 na Alexandre Lacazette dakika ya 22, huku Luka Milivojevic akiwapa Palace bao la kufutia machozi dakika ya 78.

Mashabiki wa Arsenal walitumia mitandao ya kijamii kumshambulia Sanchez, huku wakidai kwamba hakuna ulazima wa kuwa na mchezaji huyo wakati huo wana kikosi kipana ambacho kinaweza kubadili matokeo muda wowote.

Maneno hayo yalikuja mara baada ya ushindi huo mnono, hivyo wanaamini kwamba hakuna ulazima wowote wa kuendelea kumlazimisha mchezaji huyo abaki hadi pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Sanchez amekuwa akishinikiza kuondoka katika klabu hiyo tangu majira ya joto mwaka jana, lakini ikashindikana ila wakati huu wa Januari anafanikiwa mpango wake wa kuondoka kabla ya kumalizika kwa ligi majira ya joto.

Sanchez amekuwa ndani ya klabu ya Arsenal tangu mwaka 2014, akitokea klabu ya Barcelona, kwa kipindi hicho chote alichokaa amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 122 ya ligi kuu na kufunga mabao 60.

Hata hivyo, kuondoka kwa Sanchez ndani ya Arsenal, kunaifanya klabu hiyo kufikia hatua za mwisho kumalizana na kiungo mshambuliaji wa Man United, Henrikh Mkhitaryan ambaye anatarajia kufanyiwa vipimo leo hii ndani ya Emirates.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles